Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:55

Wanne wafariki katika ajali ya ndege ya Jeshi la Marekani nchini Norway


FILE - Mwezi Mei 26, 2015, photo, ndege aina ya MV-22B Osprey ikiruka eneo Babadag, Romania.
FILE - Mwezi Mei 26, 2015, photo, ndege aina ya MV-22B Osprey ikiruka eneo Babadag, Romania.

Watu wote wanne waliokuwa katika ndege ya jeshi la Marekani walifariki wakati ndege hiyo ilipoanguka katika eneo la mbali la kaskazini mwa Norway Ijumaa wakati wa mazoezi ya kijeshi yanayoongozwa na NATO, polisi katika eneo wamesema Jumamosi.

“Kwa kile polisi wanachofahamu, wanajeshi wote wanne katika ajali hiyo ni raia wa Marekani,” polisi wamesema. Waziri Mkuu Jonas Gahr Stoere alitweet kuomboleza kile alichosema kuwa ni vifo vya raia wanne wa Marekani.

Ndege hiyo aina ya MV-22B Osprey ya jeshi la Marekani ilikuwa ni sehemu ya zoezi inayoitwa Cold Response.

Huduma za uokoaji ziliwasili katika eneo la ajali kwa barabara mapema Jumamosi baada ya helikopta zilizopelekwa kushindwa kutua kutokana na hali mbaya ya hewa. Pepo za Gale-force zilikuwa zinavuma, mvua nyingi ikinyesha, na kulikuwa na hatari ya maporomoko ya theluji, kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa eneo hilo.

“Polisi walifika eneo la ajali majira ya saa 0030 GMT. Inasikitisha kuthibitisha kuwa wote wanne waliokuwa katika ndege hiyo wamefariki,” Ivar Bo Nilsson, mkuu wa operesheni za polisi Nordland, alisema katika taarifa yake.

Polisi wanachunguza sababu ya ajali hiyo japokuwa kazi yao imesitishwa kwa sababu ya hali ya hewa. Uchunguzi huo unatarajiwa kuendelea mara hali ya hewa itakapokuwa shwari.

Takriban wanajeshi 30,000 kutoka nchi 27 wameshiriki katika zoezi la kijeshi Cold Response, zoezi lililoandaliwa kutayarisha nchi wanachama wa NATO kwa ajili ya kuihami Norway.

XS
SM
MD
LG