Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:46

Wanawake wa Kilifi Kenya waeleza mradi wa ufugaji samaki ni mapinduzi kwa maisha yao


Kenya: Wanawake waeleza mradi wa ufugaji samaki ni mkombozi wa maisha yao
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:31 0:00

Kenya: Wanawake waeleza mradi wa ufugaji samaki ni mkombozi wa maisha yao

Wanawake wa vijiji vya kaunti ya Kilifi, mashariki ya Kenya wanajishuhulisha na mradi wa ufugaji samaki ambao unaleta mabadilko makubwa katika maisha yao.

Pembezoni mwa mkono wa bahari katika jimbo la Kilifi, Kenya, kunapatikana kijiji cha Kibokoni ambako wakazi wake wanategemea bahari na kilimo cha mahindi na mihogo kupata chakula.

Na moja wapo ya miradi inayowasaidia zaidi siku hizi ni mradi wa ufugaji wa samaki aina ya Tilapia wa baharini, mwatiko maarufu Milk fish, Tafi na Kamba, kwenye vidimbwi 19.

Samaki hawa wanaofahamika kupatikana katika maji baridi wamebadilishwa kustahimili maji ya baharini.

Mradi huu wa ufugaji samaki umekuwepo tangu mwaka 2011 na unasimamiwa na kikundi kinachojumuisha wanachama 55, na 38 kati yao ni wanawake.

Mradi huo unachangia katika maendeleo na usalama wa chakula kulingana na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa.

Christine Tsori ni mwenyekiti wa chama cha Umoja Self Help, anasema mradi huu umebadili maisha yao.

"Mimi mwenyewe mnaoniona hapa, ilikua niende msituni kutafuta kuni niuze huko Kilifi ndio niweza kupata fedha ili watoto wangu wasome, lakini kuopitia huu mradi naona unatupeleka vizuri, tuliangalia ule mfuo wa bahari vile wakati mwengine kuna changamoto, hakuna samaki na hivyo hapa tumebadilisha hali ya mambo," anasma Tsori.

Wanawake hao ambao sasa sasa wamekua wavuvi, wanafanya kazi bila ya kutumia vifaa vya uvuvi vya bei ghali au kuenda maji makuu na wanaweza kupata kwa urahisi samaki wa kula na kuuza kutoka vidimbwi hivi walivyovitengeza.

Kache Safari Jefwa, mama ya watoto saba, anaeeleza kuwa kamwe hakuwahi kufikiria angekua mvuvi - maisha yake yalitegemea mume wake.

Mradi huu umempa fursa kama wengine kuvua na kuuuza samaki, fedha wanazopata wanatumi kukimu mahitaji ya familia zao ikiwemo kuelimisha watoto wao.

"Pesa nikizipata kutoka huku ambazo ninagawiwa na wenzangu ninapeleka kwa mzee na kwa watoto wangu kusoma. Tunasaidiana na mzee," anasema Jefwa

Mradi huu wa Blue Empowerment unaotekelezwa na masharika na taasisi, mbali mbali nchini, na unaongozwa na shirika la African Centre for Technology na taasis ya utafiti wa viwanda na maendeleo Kenya KIRDI, unalenga kubadili maisha ya wanawake wavuvi vijijini kupitia teknlojia hii ya kufuga samaki walioboreshwa kustahamili hali ngumu ya mazingira

Dk. Linus Kosambo mtafiti wa kisayansi kutoka taasis ya KIRDI kwa hivi sasa wanaagizia samaki kutoka nje, lakini wakifanikiwa na mradi huu wataweza kupunguza sana fedha zinazokwenda nje.

"Tuko na defeceit ya kama tani elfu 300 ile tunayotoa kutoka nje. Kama tutaweza kupounguza idadi hiyo tutakua tuimeisaidia nchi sana kimapato kutokana na pesa tunazotumia kununua kutoka China pamoja na samaki duni kutoka zile nchi nyingine tunazoziita rejects, hazitakuja hapa nchini kwetu. Sasa mradi kama huu watu wa sayansi wakishabuni, na kuonesha kiteknolojia kuwa inaweza kuterndeka. Basi wale washika dau wote wanabidi kushirikiana pamoja na tuone kwamba inaweza kupanuka." anasema Dk. Kosambo

Wanawake hawa wamekua wakivua kilo 55 za samaki katika kila kidimbwi, wateja wakuu ikiwa ni hoteli za kitalii Pwani ya Kenya

Licha ya kwamba mradi huu kuzalisha chakula na ajira kwa wanakibokoni, lakini bado hawana mashine ya kusindika na kuongeza thamani samaki wao.

Hata hivyo hatua ya serekali ya Kenya kutenga wizara maalum kushughulikia uchumi wa blue, unawapa matumaini.

Michael Keah mshauri wa kundi la Self Help anasema kama wameunda wizara hiyo basi itawasaidia maana awali ilikua mkifanya maombi hupati msaada kwa sababu hakuna wizara maalum ya hilo, basi hapo mafanikio

Ripoti imetayarishwa na Amina Chombo, Sauti ya Amerika

XS
SM
MD
LG