Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 21:55

Wanawake vijijini Tanzania wakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi na vifaa tiba


Mwanamukuu Fadhili with Mariam Hassan speaking with Voice of America in Tanga, Tanzania.
Mwanamukuu Fadhili with Mariam Hassan speaking with Voice of America in Tanga, Tanzania.

Kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi na vifaa tiba katika hospitali za vijijini nchini Tanzania kumetajwa kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazo wakabili wanawake kutohudhuria kliniki hali inayo pelekea kujifungulia majumbani.

Upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika jamii licha ya umuhimu wake lakini bado wanawake na wasichana wanaendelea kupitia vipindi vigumu na hivyo kuwatia hofu hasa pale inapofikia wakati wa kujifungua huku malalamiko yao wakiyaelekeza kwa serikali na wanasiasa ambao wamekuwa wakidai kutetea maslahi ya wanawake na wasichana.

Serikali ya Tanzania imeweka mipango kuwa kila mwanamke anapo kwenda kujifungua atapatiwa huduma bure za uzazi hali ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikikinzana na kauli zao na kupelekea jamii kutofahamu ni huduma gani ambazo viongozi wanazizungumzia. Mariamu Hassani mkazi wa Gombero Tanga anasema licha ya kwenda kliniki kila mwezi lakini bado hawapatiwi elimu yoyote inayoweza kuwasaidia kufahamu ni huduma gani zinatolewa bure na nini mchango wao.

Aidha Serikali ilitenga kiasi cha shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika mwaka wa fedha 2022/2023 huku Bilioni 74.3 zikiwa tayari zimetolewa katika kumaliza changamoto ya upungufu wa dawa na vifaa tiba nchini humo suala ambalo wanawake wamebaki na maswali wapi vifaa hivyo vimepelekwa kwasababu hata wanapotakiwa kwenda katika hospitali ya mkoa wamekuwa wakikosa baadhi ya vipimo na kutakiwa kwenda katika hospital binafsi.

Pendo Faustini mkazi wa Gombero akizungumza na sauti ya Amerika amesema serikali iweke vifaa tiba katika hospitali ili kuwapunguzia kuhangaika wakati wanapo kwenda kufuata huduma

Hata hivyo Mwanamkuu Fadhili Mama wa nyumbani anayeishi Manza bay mkoani Tanga amesema wanapo kwenda hospitali wanatakiwa kiasi fulani cha fedha lakini huishia kuandikiwa na kutakiwa kununua dawa nje ya hospitali suala ambalo anaitaka serikali iliangalie kwa kina hususani kwa wanawake wanaoishi vijijini ambao wamekuwa wakisahaulika kwa miaka mingi.

Bado wanawake wanaoishi vijijini matumaini yao yapo kwa serikali kuhakikisha wanaondosha matabaka baina ya mjini na vijijini kwa kuwapelekea huduma zitakazo wafanya wajione hawajabaguliwa amemalizia kusema Mwanamkuu.

Imeandaliwa na Amri Ramadhani Sauti ya Amerika Dar es Salaam.

XS
SM
MD
LG