Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:10

Wanariadha watakaowakilisha Kenya mjini London watajwa


Bingwa wa Olimpiki na mawnariadha wa Kenya David Rudisha anaonekana hapa katika mashindano ya awali.
Bingwa wa Olimpiki na mawnariadha wa Kenya David Rudisha anaonekana hapa katika mashindano ya awali.

Shirikisho la wanariadha nchini Kenya, siku ya Jumamosi lilitoa orodha ya majina ya wanariadha watakaowakilisha nchi hiyo kwenye mashindano ya kimataifa yatakayofanyika mjini London, Uingereza, kati ya tarehe 4 na 13,  Agosti mwaka huu.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, shirikisho hilo lilitaja majina yao baada ya mashindano ya siku mbili ya kutafuta mabingwa wa taifa, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyayo Stadium, mjini Nairobi.

Emmanuel Korir, ambaye ni mkenya anayeishi Marekani, Kipyegon Bett, Furguson Rotich na bingwa wa dunia wa mbio za mita 800, ni baadhi ya wanariadha watakaoiwakilisha Kenya kwenye mashindano hayo.

Wengine ni pamoja na bingwa wa mara nne wa mbio za mita 3,000 za kuruka viunzi, Ezekiel Kemboi na bingwa wa olimpiki katika mbio hizo hizo, Conslesus Kipruto.

Aidha, Purity Kirui, na Celphine Chespo wataiwakilisha Kenya katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi.

Gazeti hilo limeandika kuwa mashindano hayo ya matayarisho yalikuwa na ushindani mkubwa huku baadhi ya waliotarajiwa kufuzu wakishindwa na wanariadha ambao itakuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki kwenye kinyan'anyiro hicho cha kimataifa.

XS
SM
MD
LG