Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:45

Wananchi wana matumaini uchaguzi wa Niger Jumapili utaweka historia


Wanajeshi wa Nigeria wakilinda doria nje ya uwanja wa ndege wa Diffa Kusini mashariki mwa Niger karibu na mpaka wa Nigeria Disemba 23, 2020.
Wanajeshi wa Nigeria wakilinda doria nje ya uwanja wa ndege wa Diffa Kusini mashariki mwa Niger karibu na mpaka wa Nigeria Disemba 23, 2020.

Wananchi wa Niger wana matumaini ya kuweka historia Jumapili watakapo kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge ambao kwa mara ya kwanza utaruhusu kukabidhiana madaraka kwa amani tangu kupata uhuru miaka 60 iliyopita kutoka Ufaransa.

Kuna wagombea 30 wanaopigania kiti cha rais lakini mwandishi wa idhaa ya Hausa ya Sauti ya Amerika Mahmud Lalo anaripoti kutoka Niamey kwamba baadhi ya watu hawana hamu na uchaguzi huo kutokana na kuondolewa kwa kiongozi mkuu wa Upinzani.

Taswira ya mji mkuu Niamey imebadilika kutokana na mabango makubwa ya matangazo ya kisiasa na picha za wagombea uchaguzi, zinazowavutia watu wanaopita huku kampeni zikimalizika mnamo siku moja.

Kuna viti 171 vya bunge vinavyo gombaniwa kwenye uchaguzi huu na wagombea kiti cha urais wako 17 ambao wanashindana kuchukua nafasi ya Mahamadou Issoufou anaekamilisha muhula wake wa pili.

Lakini licha ya kampeni hizo inaonekana watu wengi katika mji mkuu hawana hamu na uchaguzi huo. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Nasirou Saidou anasema kuna mambo mengi yaliosababisha watu kutojali na moja wapo ni matayarisho.

Nasirou Saidou, mchambuzi wa masuala ya kisiasa anasema : "Niger imeshaanda uchaguzi kadhaa mnamo miaka 30 iliyopita, lakini hii ni mara ya kwanza tuna uchaguzi ambao haujatayarishwa vilivyo.

Zaidi ya hayo Hama Amadou wa chama cha upinzani cha Lumana aliyekuwa Spika wa zamani na Waziri Mkuu mara mbli anayechukuliwa kuwa mshindani mkubwa kwenye uchaguzi wa urais ameondolewa kwa madai kwamba alihukumiwa kifungo cha miezi 12 kutokana na kashfa ya biashara haramu ya Watoto hapo mwaka 2017.

Hama Amadou
Hama Amadou

Alikanusha tuhuma hizo na baadae kupewa msamaha na rais. Hata hivyo Bana Ibrahim wa chama chake anaeleza matumaini ya ushindi wa upinzani.

Bana Ibrahim, afisa wa chama cha Lumana anaeleza : "Mahakama ya kikatiba imemondowa Hama Amadou lakini hiyo haimanishi kwamba hatutashiriki kwenye uchaguzi. Kile tunacho hitaji Niger ni mabadiliko, kwa hivyo hata kama kama hagombanii kiti cha urais tunatazamia kuunda muungano, ni mmoja wapo wa viongozi wa upinzani katika duru ya pili.

Kutakuwa na duru ya pili pindi hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 za kura. Bazoum Muhamed waziri wa zamani wa mambo ya nje wa chama tawala cha PNDS Tarayya , na mshirika wa karibu wa Rais Issoufou anatarajiwa kupata ushindi katika duru ya kwanza anasema Tahitou Garka ambaye ni afisa muandamizi wa chama tawala.

Tahirou Garka, afisa muandamizi wa chama cha PNDS Tarayya anasema : "Tutapata ushindi kwa kishindo kikubwa katika duru ya kwanza kwa sababu tulipata zaidi ya asilimia 50 za kura mnamo uchaguzi wa karibuni wa serikali za mitaa. Na kwa vile Bazoum anaungwa mkono na zaidi ya vyama 50, basi tunahakika tutapata zaidi ya asilimia 60 za kura au hata zaidi.

Niger ni mojawapo ya mataifa maskini duniani licha ya utajiri mkubwa wa madini, inakabilwa na matatizo makubwa ya kiuchumi na hasa mashambulio ya wanamgambo wenye itikadi kali za kislamu kutoka nchi jirani za Mali na Nigeria.

Wafanyabiashara wakiuza bidhaa katika mji wa Diffa, Kusini mashariki mwa Niger karibu na mpaka wa Nigeria, on Disemba 23, 2020, karibu na uchaguzi mkuu wa Disemba nchini Niger. (Photo by Issouf SANOGO / AFP)
Wafanyabiashara wakiuza bidhaa katika mji wa Diffa, Kusini mashariki mwa Niger karibu na mpaka wa Nigeria, on Disemba 23, 2020, karibu na uchaguzi mkuu wa Disemba nchini Niger. (Photo by Issouf SANOGO / AFP)

Na zaidi ya hayo mnamo miaka ya hivi karibuni taifa hilo la Sahel limekumbwa na ukame unaozidisha umaskini na kusababisha vijana kuondoka kuelekea nchi za Ulaya. Hivyo yeyote atakae shinda anakabiliwa na changamoto hizo zote na matarajiyo ya mageuzi kutoka kwa wananchi waliowengi.

XS
SM
MD
LG