Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:10

Wabunge wa Ufaransa watoa heshima bungeni kwa wanajeshi 13 waliouawa Mali


Helikopta aina ya Tiger kwenye uwanja Kaskazini ya Mali tayari kupa
Helikopta aina ya Tiger kwenye uwanja Kaskazini ya Mali tayari kupa

Wabunge wa Ufaransa wametoa heshima zao bungeni, Jumanne kwa wanajeshi 13 walofariki kaskazini mwa Mali kutokana na ajali ya helikopta iliyotokea kaskazini mwa nchi walipokua bwanakwenda kuwasaka magaidi.

Hii ni idadi kubwa ya wanajeshi wa Ufaransa kufariki pamoja tangu nchi hiyo kuingia Mali 2013 ili kupambana na ugaidi.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Florence Parly, akizungumza na waandishi habari mjini Paris, ametowa rambi rambi kwa familia za wanajeshi walofariki, akisema, wanajeshi wenzao wameweza kufika katika eneo la ajali na kupata mili ya wanajeshi wote13 walofariki.

Parly amesema maombolezi ya kitaifa yatafanyika mjini paris kwenye uwanja wa Les Invalides hivi karibuni.

Amesema helikopta hizo ziligongana zilipokua zinasafiri chini kwa chini magharibi kuwasaidia wanajeshi walokuwa ardhini wakifukuzana na wanamgambo wa kislamu.

Kufuatana na ripoti ya Shirika la Habari la AFP ni kwamba helikopta ya mashambulizi ya aina ya Tiger iligongana na nyingine ya kusafirisha wanajeshi aina ya Cougar, zilipokua zinajaribu kuwafuata magaidi walokuwa kwenye pikipiki na lori wakikimbia.

Helikopta aina ya Tiger iliyogongana kaskazini ya Mali
Helikopta aina ya Tiger iliyogongana kaskazini ya Mali

Vifo hivyo vinafikisha idadi ya wanajeshi wa Ufaransa walouliwa tangu nchi hiyo kupeleka wanajeshi wake Mali kusaidia kupambana na magaidi 2013 kufikia 41.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametoa rambi rambi zake na kusema wanajeshi hao wanefariki “kwa ajili ya Mali na nchi zote za Sahel, pamoja na Ufaransa.” Ajali hiyo kwa hivyo ni pigo kubwa ambapo ni mbaya kabisa ya wanjeshi wengi wa Ufaransa kufariki katika operesheni tangu vita vya Lebanon mweaka 1983.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameahidi kwamba atatangaza hatua mpya katika wiki chache zijazo kuimarrisha vita dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali za kislamu huko Sahel, alipowapokea marais wa Mali, Chad na Niger kwenye ikulu ya Elysee.

Ufaransa ina kikosi kinachofahamika kama Barkhane, cha wanajeshi 4 500 huko Mali. Na vikosi vingine katika mataifa mengine ya Afrika Magharibi, ya Burkina Faso Niger, Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika juhudi za kupambana na wanamgambo wa kislamu katika kanda hiyo ya Sahel.

Kwa siku 15 za Novemba wanajeshi wa Ufaransa wamekuwa wakipiga doria na kufanya msako kote katika eneo la kaskazini mwa Mali ambako hakuna mamlaka ya usalama kutoka serikali kuu.

Kanali Lemerie anaeongoza operesheni hiyo anasema hilo ni eneo zuri la usalama kwa magaidi.

“Hilo ni eneo ambalo ni rahisi kuvuka mpaka kutoka nchi moja hadi nyingine kwa urahisi. Na ni eneo gumu kufika lisilo na njia za kawaida. Kwa hivyo ni mahala pazuri kabisa kiujificha na kupanga njama zao,” amesema Kanali Lemerie.

Wanajeshi wa Mali wakipiga doria na wanajeshi wa Ufaransa katika mji wa Menaka, Mali
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria na wanajeshi wa Ufaransa katika mji wa Menaka, Mali

Hii ni mara ya kwanza tangu kufikia huko Mali ambapo wanajeshi wa Ufaransa wanashirikiana na wanajeshi wa Burkina Faso, Niger na Mali kupiga doria kwa pamoja. Operesheni hiyo yenye wanajeshi 1 400 ina lengo la kuwasaka na kuwaondowa wanamgabo kutoka eneo hilo. magaidi.

Luteni Bambara Abdou Gafao mwanajeshi wa Burkina Faso analiambia shirika la habari la AFP kwamba hadi hivi karibuni wanajeshi hawakuthubuti kuingia katika eneo hilo. Na hivi sasa wanajaribu kupata imani yao

"Tuna nia ya kuwaonesha wananchi kwamba tuko hapa kuwalinda na tuko tayari kuwasaidia kupigana na maadui," amesema Abdou Gafao.

Wanajeshi wana kazi ngumu ya kuwatafuta wanamgambo hao ambao wanajingiza kwa urahisi miongoni mwa wananchi na matokeo yake wanajeshi wa Ufaransa wanawashuku wananchi wote katika eneo hilo, na hapo mkuzusha hali ya kutoaminiana. Kwani katika juhudi zao wanalazimika kuwakagua wakazi wote huku wakihakikisha wanafahamu wako huko kuwasaidia.

Wanapoendelea na juhudi hizo mataifa hayo ya Sahel yanakabiliwa na changamoto chungu nzimaikiwa matatizo ya uchukuzi utaalamu pamoja na namna wanajeshi wan chi hzio zinazopakana wanavyoweza kushirikiana, utaratibu ambao unadhihirisha ungali unazusha mivutano.

XS
SM
MD
LG