Ufaransa ina takriban wanajeshi 2,400 nchini Mali, ikiwa ni sehemu ya wanajeshi wake 4,300 walioko Afrika Magharibi wanaolenga kuleta utulivu katika eneo la Sahel dhidi ya tishio linaloongezeka la wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali.
Utawala wa kijeshi nchini humo umetaka kuondoka mara moja kwa vikosi vya Ufaransa na Ulaya, siku moja baada ya Ufaransa kutangaza kuwa itaondoa wanajeshi wake katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa tangazo la kujiondoa Alhamisi, akisema kwamba litafanyika katika kipindi cha miezi sita
Iwapo Ufaransa inataka kuondoka, ni lazima ifanye hivyo mara moja, bila suala la miezi minne au sita, muandamanaji Fatim Touré alisema wakati wa maandamano ya Jumamosi.
"Tunaunga mkono viongozi wetu. Ufaransa isibaki tena Mali."aliongeza.
Tangu mapinduzi ya Agosti 2020, Mali imekuwa ikiongozwa na Kanali Assimi Goita.