Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 14, 2025 Local time: 01:50

Wanajeshi 8 wa Mali wauwawa katika mapambano na wanamgambo wa Kiisalm


Wanajeshi wa Mali wakipiga doria na wanajeshi wa Ufaransa katika mji wa Menaka, Mali
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria na wanajeshi wa Ufaransa katika mji wa Menaka, Mali

Wanajeshi wanane wa Mali waliuawa, wengine 14 kujeruhiwa na wanne hawajulikani walipo kufuatia mapambano na wanamgambo wa Kiislamu

Wanajeshi wanane wa Mali waliuawa, wengine 14 kujeruhiwa na wanne hawajulikani walipo kufuatia mapambano na wanamgambo wa Kiislamu wenye silaha kaskazini mashariki mwa taifa hilo la Afrika Magharibi siku ya Ijumaa, wizara ya ulinzi ilisema.

Wizara hiyo ilisema Ijumaa jioni kwamba makundi ya wanajihadi wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki walikuwa wamekibana kikosi hicho, lakini jeshi, likisaidiwa na jeshi la anga, liliwaua 57 kati yao katika eneo la mpakani karibu na Burkina Faso.

Mali, Burkina Faso na Niger wanajitahidi kuwadhibiti wanamgambo wenye silaha wanaohusishwa na al Qaeda na Islamic State ambao wanadhibiti baadhi ya maeneo katika mpaka wa Sahel huko Afrika Magharibi ambao ina ukubwa kuliko Ujerumani.

Shambulio hilo limetokea wakati utawala wa kijeshi wa Mali siku ya Ijumaa uliitaka Ufaransa kuondoa wanajeshi wake katika eneo lake "bila kuchelewa, na kutilia shaka mpango wa Paris wa kuondoka katika miezi minne hadi sita na kuangazia kuvunjika kwa uhusiano kati ya Paris na koloni lake la zamani.

XS
SM
MD
LG