Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 29, 2024 Local time: 19:39

Wanamgambo wafanya shambulizi Dagestan


Wanamgambo wenye silaha wameshambulia makanisa mawili ya Orthodox, na kituo cha polisi katika jamhuri ya kusini mwa Russia, Dagestan, ambapo kasisi ameuwawa na maafisa sita wa polisi, shirika la habari la serikali ya Russia, RIA Novosti limeripoti Jumapili.

Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Ugaidi ya Russia, imesema katika taarifa kasisi wa Kanisa la Orthodox la Russia, na maafisa wa polisi wameuwawa katika shambulizi la kigaidi.

Wizara ya Mambo ya Ndani wa Dagestan imesema kundi la watu waliokuwa na silaha lilifyatua risasi kwenye kanisa katika jiji la Derbent, lililo kwenye Bahari ya Caspian.

Washambuliaji wamekimbia na msako mkali unaendelea kuwatafuta, taarifa kutoka kwa wizara hiyo imesema. Wizara imesema wanamgambo wawili wa kundi hilo wameuwawa.

Forum

XS
SM
MD
LG