Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:52

Wanamgambo wa kiislamu wauteka mji mmoja wa Mali


Ramani ya Mali
Ramani ya Mali

Wanamgambo wa kiislamu wenye uhusiano na kundi la Islamic State wameuteka mji wa Mali wa Tidermene, na kuutenga zaidi mji mkuu wa mkoa huo, Menaka, katika eneo ambalo karibu lote liko chini ya udhibiti wao, maafisa na mashahidi waliliambia shirika la habari la AFP Jumatano.

Kutekwa kwa mji wa Tidermene kunafuatia mapigano ya miezi kadhaa ya kundi la Islamic State katika eneo la Greater Sahara kwa kudhibiti kijiji cha kaskazini mashariki chenye wakazi walio chini ya 1,000 umbali wa kilomita 75 kaskazini mwa Menaka.

Maeneo madogo yote ya utawala wa mkoa huo yako chini ya udhibiti wa kundi hilo.

“Tidermene iko mikononi mwa kundi la Daesh,”, afisa aliyechaguliwa katika mji huo, ambaye alikimbilia Menaka ameiambia AFP.

Amesema wanamgambo hao wanagawa vitabu vya Quran kwa wakazi na wanatembea karibu na mji wakiwa na silaha.

Afisa mwingine aliyechaguliwa ameiambia AFP kwamba wanamgambo hao waliwaambia wakazi wa kijiji kuendelea na shughuli zao kama kawaida, lakini wajiandae kuanza kulipa zaka, ambao ni ushuru katika dini ya Kiislamu.

XS
SM
MD
LG