Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, tukio hilo limetokea baada ya mmoja wa wanajeshi hao kushambulia mwenzake na kumpiga risasi, kabla ya kujipiga risasi mwenyewe, jeshi la Afrika Kusini la National Defence Force, SANDF limesema, kupitia taarifa.
Taarifa imeongeza kuwa maafisa hao wamekufa wakiwa sehemu ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO, ambao tayari wameanza kuondoka nchini humo. Takriban wanajeshi 2,900 kutoka Afrika Kusini wanashika doria DRC, kama sehemu ya kikosi cha SADC, kilichotumwa na serikali kukabiliana na waasi wa M23.
Wanajeshi wengine wawili wa Afrika Kusini waliuwawa mwezi uliopita kupitia shambulizi la kombora, tukio lililopelekea vyama vya upinzani vya Afrika Kusini kudai kwamba walitumwa DRC bila kuwepo kwa mipango ya kutosha ya kiufundi.
Forum