Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:41

Wanajeshi watano wauwawa na Alshabab kwenye kambi Somalia


Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia.
Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia.

Wanamgambo wa Kiislamu wa al Shabaab Ijumaa waliwaua wanajeshi watano katika kambi ya jeshi ya Somalia katika mji uliochukuliwa  tena hivi karibuni na serikali, wanajeshi na wakaazi walisema.

Shambulio hilo hatimaye lilizimwa, afisa mmoja katika kambi ya katikati mwa Somalia ya mji wa Galcad aliiambia Reuters. Alisema waliofariki ni pamoja na naibu kamanda wa kambi hiyo, ambaye alikuwa sehemu ya kitengo kilichopatiwa mafunzo na Marekani kilichokuwa hapo.

Shambulio hilo linadhihirisha tishio kubwa la al-Shabaab kwa wanajeshi wa Somalia, hata baada ya mashambulizi ya serikali yaliyoanzishwa mwaka jana kupata mafanikio makubwa dhidi ya wanamgambo wenye uhusiano na al-Qaeda.

Wapiganaji wa Al Shabaab waliivamia kambi ya Galcad mapema siku ya Ijumaa, na kulipua mabomu yaliyotegwa kwenye magari na kufyatua silaha zao, Kapteni Issa Abdullahi alisema.

Kambi hiyo inaendeshwa na Danab, kitengo cha makomandoo waliopatiwa na Marekani ambao wameshiriki katika mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao.

XS
SM
MD
LG