Katika kukabiliana na hali hiyo, polisi na vikosi vya jeshi vilisambazwa kwa haraka katika eneo hilo, kuweka uzio na kuanza msako.
Tukio hilo ambalo hakuna kundi la waasi limedai kuhusika nalo, ni la karibuni kabisa katika mfululizo wa mapigano makali.
Siku moja kabla, mapigano mawili tofauti katika wilaya ya Kulgam yalisababisha vifo vya wanajeshi wawili wa India na watu sita wanaoshukiwa kuwa wanamgambo, ripoti za polisi zinaeleza.
Mapema siku hiyo hiyo, wanamgambo walifyatua risasi kwenye kambi ya jeshi katika wilaya ya Rajouri na kumjeruhi mwanajeshi mmoja.
Kashmir inapatikana katika milima Himalaya kati ya Pakistan na India, eneo ambalo limekuwa likigombaniwa na nchi hizo tangu mwaka wa 1947.
Forum