Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 18:06

Wanajeshi wa Russia washtumiwa kwa mateso na mauaji ya kiholela katika mji wa Ukraine wa Mariupol.


Wanajeshi wanaounga mkono Russia wakikagua mitaa katika mji wa bandari wa Mariupol, kusini mwa Ukraine. April 7, 2022. Picha ya Reuters.
Wanajeshi wanaounga mkono Russia wakikagua mitaa katika mji wa bandari wa Mariupol, kusini mwa Ukraine. April 7, 2022. Picha ya Reuters.

Ukraine Jumatatu imesema maelfu ya watu waliuawa katika uvamizi wa Russia kwenye mji wa kusini mashariki wa Mariupol, huku mpatanishi wa taifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu akiwashtumu wanajeshi wa Russia kwa mateso na mauaji ya kiholela katika eneo hilo.

Reuters imethibitisha uharibifu mkubwa katika mji wa Mariupol lakini haikuweza kuthibitisha madai ya uhalifu au makadirio ya wale waliouawa katika mji huo muhimu ambao upo kati ya eneo la Crimea linalotawaliwa na Russia na maeneo yanayoshikiliwa na waasi wanaotaka kujitenga ambao wanaungwa mkono na Russia.

“Mariupol imeharibiwa, kuna maelfu ya waliokufa, lakini pamoja na hivo, Warussia hawakomi kusitisha mashambulizi yao,” Rais Volodymyr Zelensky amesema katika hotuba ya video kwa wabunge wa Korea Kusini bila kutoa maelezo zaidi.

Kiongozi wa Jamuhuri ya watu wa Donetsk inayoungwa mkono na Russia, Denis Pushilin, ameliambia shirika la habari la Russia RIA Jumatatu kwamba zaidi ya watu 5,000 huenda waliuawa huko Mariupol, akisema wanajeshi wa Ukraine ndio walihusika na mauaji hayo.

Akinuku takwimu za utawala wa jiji la Mariupol, mpatanishi wa Ukraine anayehusika na haki za binadamu Lyudmyla Denisova amesema wakazi 33,000 walirudishwa Russia au kwenye maeneo yanayoshikiliwa na waasi wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Russia.

Russia Jumapili ilisema iliwahamisha watu 723,000 kutoka Ukraine tangu kuanzisha kile ilichokiita “ operesheni yake maalum.”

Moscow inakanusha madai ya kushambulia raia.

XS
SM
MD
LG