Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 18:04

Wanajeshi Mali wapindua serikali.


Wanajeshi wa kundi la waasi la MNJ huko Niger ambalo linaongozwa na Watuareg.
Wanajeshi wa kundi la waasi la MNJ huko Niger ambalo linaongozwa na Watuareg.

Askari waasi wamepindua serikali wakidai wamechoshwa na uasi wa Watuareg.

Askari waasi wa Mali wanasema wamemwondoa madarakani Rais Amadou Toumani Toure wiki chache tu kabla ya muda wake kumalizika.

Kundi moja la wanajeshi lilijitokeza katika televisheni ya taifa alhamisi asubuhi baada ya usiku wa mashambulizi ya bunduki katika eneo la makazi ya rais .

Msemaji wa wanajeshi hao alisema wameumaliza utawala usiofanya kazi , wameisimamisha katiba kwa muda na kuunda kamati mpya ya kutawala nchi.

Wanajeshi hao walionyesha kuchoshwa na rais jinsi anavyokabiliana na kuanza tena kwa uasi wa Watuareg huko kaskazini mwa Mali. Waasi hao wameteka miji kadhaa na mapigano yamesababisha maelfu ya raia wa Mali kukimbia nyumba zao.

XS
SM
MD
LG