Wameyasema hayo wakati wa kongamano kuhusu elimu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kabla ya kufanyika kwa mkutano wa baraza kuu la Umoja huo , ambapo viongozi wanatarajiwa kutoa ahadi zao za kuhakikisha kwamba wanafunzi hawabaki nyuma kielimu kuanzia barani Afrika hadi hapa Marekani.
Mshindi wa tuzo ya Nobel mwaka 2014 kutoka Pakistan Malala Yousfzai, ambaye pia ni mjumbe wa amani wa UN wakati wa kikao hicho alisema kwamba miaka 6 iliyopita alisimama tena mbele ya baraza hilo akiomba sauti ya msichana aliyepigwa risasi wakati akitafuta elimu nchini mwake isikilizwe.
Ameongeza kusema kwamba wakati huo viiongozi waliahidi kuhakikisha kwamba kila mtoto anapata elimu kufikia 2030, na kwamba inahuzunisha kuona hatua zilizopigwa. Mwanaharakati wa vijana kutoka Nigeria Karimot Odebode kwa upende wake alisema kwamba hawatachoka hadi pale kila mwanafunzi kutoka kila kijiji ulimwenguni atakapo pata elimu.