Wakiwa wamebeba mabango yenye maneno ya “ msilete janga la mazingira", msiiharibu Afrika kwa gesi pamoja na “, "kuangamiza nishati ya gesi", wameandamana nje ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira wa COP27 nchini Misri, katika mji wa Sharm al Sheikh.
Waandamanaji hao wanadai kuwa washiriki wa mkutano huo wamekwepa kuzungumzia athari za nishati kutokana na mafuta ghafi. Wameongeza kusema kwamba washiriki walihudhuria kwa hisani ya makampuni makubwa ya nishati.
Wamesema pia kwamba washiriki hao wanaweka maisha ya maelfu ya watu hatarini. Alhamisi Umoja wa Ulaya ulitoa mapendekezo kadhaa kama vile kubuni mfuko wa kuyasaidia mataifa masikini kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na kupunguza uzalishaji wa nishati chafu yenye kuharibu mazingira.