Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:41

Wanafunzi 22 wazama maji Sudan


Ramani ya Sudan
Ramani ya Sudan

Wanafunzi wasiopungua 22 wamezama maji Jumatano baada ya boti iliyokuwa na watu zaidi ya 40 kuzama ilipokuwa inakatiza mto Nile Kaskazini mwa Sudan, shirika la habari la serikali ya Sudan (SUNA) limesema.

Vikosi vya kuwalinda raia viliendelea kuwatafuta wasafiri hao katika eneo hilo la mto, lakini mpaka sasa hawajafanikiwa kupata mwili wowote, Shirika hilo limeeleza.

Pia mfanyakazi wa kike wa hospitali alikuwa kati ya wale waliozama

Watoto hao walikuwa wakielekea shuleni wakati boti hilo lilipopinduka na kuzama katika mto Nile ambao umefurika kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Sudan.

Tukio hilo limetokea kilomita 750 kaskazini mwa mji wa Khartoum.

Kulingana na shirika la habari la AFP, kikosi cha waokoaji kinaendelea na shughuli za kutafuta miili ya waliokufa.

Shirika la habari la serikali ya Sudan SUNA, linaripoti kwamba ajali hiyo imesababishwa na hitilafu kwenye ingini ya boti kutokana na mawimbi mazito ya mto, wakati boti hilo lilipofika katikati ya mto.

Kulingana na Ibrahim Hassan, watoto tisa wamenusurika.

Shirika la habari la SUNA linasema kwamba boti lilikuwa limepakia kuzidi kiasi. Kando na kubeba Zaidi ya watoto 40, lilikuwa pia limebeba gunia 30 za viazi tamu, gunia kumi za nafaka na mwanamke aliyekuwa akifanya kazi katika hospitali moja nchini Sudan.

Wanakijiji katika sehemu hiyo wanategemea usafiri wa boti za mbao kuvuka mto Nile.

Ajali za boti hutokea mara nyingi katika mto Nile, nchini Sudan.

Mnamo mwezi Agosti mwaka 2000, watoto 50 waliaga dunia baada ya boti walilokuwa wameabiri kupindukia katika mto Nile, kilomita 350 kusini mashariki mwa Khartoum.

Watu 13 walaiaga dunia katika ajali sawia na hiyo mnamo septemba mwaka 2014 boti lao lilipozama kaskazini mwa Khatoum.

Mvua nyingi inaendelea kunyesha nchini Sudan na kuongeza kiwango cha maji katika mto Nile. Mafuriko pia yameshuhudiwwa katika mji mkuu wa Khartoum na kutatiza huduma za usafiri na umeme.

XS
SM
MD
LG