Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 03:14

Waliotenda uhalifu dhidi ya waandamanaji Syria mwaka 2012 wamekamtwa


Waandamanaji waliokuwa wanapinga serikali katika mji wa Habit, nchini Syria. May 11, 2012.
Waandamanaji waliokuwa wanapinga serikali katika mji wa Habit, nchini Syria. May 11, 2012.

Mamlaka nchini Ujerumani na Sweden wametangaza kuwakamata watu wanane wanaoshukiwa kutenda uhalifu dhidi ya ubinadamu kuhusiana na msako kwa waandamanaji wa Amani m waka 2012 nchini Syria.

Waendesha mashtaka nchini Ujerumani wamesema kwamba miongoni mwa waliokamatwa nchini humo ni watu wasiotambuliwa kama wasyria wenye asili ya palsetina wasiokuwa na utaifa na nchi yoyote, ambao walikuwa na mahusiano na wanamgambo wa Syria.

Mwingine ni raia wa Syria ambaye alikuwa ni afisa wa ujasusi wa serikali.

Waendesha mashtaka wamesema kwamba waliokamatwa walishiriki katika msako mbaya dhidi ya maandamano ya amani katika wilaya ya Al-Yarmouk, mji mkuu wa Damascus, nchini Syria.

Washukiwa watatu waliokamatwa nchini Sweden walikuwa sehemu ya kundi hilo la wanamgambo sawa na waliokamatwa Ujerumani.

Forum

XS
SM
MD
LG