Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:43

Walinda amani wa umoja wa mataifa washutumiwa Sudan Kusini


watoto waliokoseshwa makazi ndani ya nchi sudan kusini
watoto waliokoseshwa makazi ndani ya nchi sudan kusini

Walinda Amani walitelekeza nafasi zao na kisha walitumia gesi ya kutoa machozi kwa raia waliozingirwa ambao walikuwa wakitafuta makazi ya muda kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa, kundi linalosaidia raia walioko kwenye mzozo

Kundi moja la haki za binadamu linasema kwamba walinda Amani wa Umoja wa Mataifa walishindwa katika operesheni zao za kuwalinda raia nchini Sudan Kusini wakati wa mlipuko wa mapigano nchini humo mwezi Julai.

Walinda Amani walitelekeza nafasi zao na kisha walitumia gesi ya kutoa machozi kwa raia waliozingirwa ambao walikuwa wakitafuta makazi ya muda kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa, kundi linalosaidia raia walioko kwenye mzozo, -Center for Civilian in Conflict-CIVIC, lenye makao yake hapa marekani lilisema katika ripoti yake iliyotolewa jana jumatano.

Umoja wa Mataifa unahitaji kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika kuchukua hatua dhidi ya viwango vya mapungufu ya walinda Amani wake, ilisema ripoti hiyo.

Sudan Kusini iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya kipindi cha miaka miwili baada ya kujipatia uhuru mwaka 2011, wakati rais salva Kiir alipomshutumu makamu rais wake wa zamani, Riek Machar kwa kupanga mapinduzi.

Bwana Machar alirudi kwenye mji mkuu juba mwaka huu baada ya mkataba wa Amani ulipoafikiwa mwaka jana, lakini mapigano mapya kati ya vikosi vya Machar na wanajeshi wa serikali wanaomtii Kiir yalizuka mwezi Julai. Mamia ya watu walikufa katika mapambano hayo.

XS
SM
MD
LG