Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:02

Wakimbizi Waliopo Tanzania Kupunguziwa Mgao Wa Chakula: WFP


Wakimbizi wa Burundi katika kambi iliyopo hukoTanzania.
Wakimbizi wa Burundi katika kambi iliyopo hukoTanzania.

Idara ya Umoja wa mataifa ya mpango wa chakula duniani -WFP inasema inapunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi 320,000 wanaoishi kaskazini-magharibi mwa Tanzania kutokana na upungufu wa msaada wa ufadhili. WFP ilisema katika taarifa ya Jumapili kwamba inahitaji haraka msaada wa dola milioni 23.6 ili kukidhi mahitaji ya chakula na lishe kwa wakimbizi hadi mwezi Disemba.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP wakimbizi walioathirika wengi wanatoka nchini Burundi na Congo. Michael Dunford, mwakilishi wa WHO nchini Tanzania alisema “kuna umuhimu wa kupunguza mgao zaidi wa chakula” kama wafadhili hawatajibu haraka.

WFP inahitaji haraka msaada wa chakula.
WFP inahitaji haraka msaada wa chakula.

WFP inasema ugawaji wa chakula ulipunguzwa kwa mwezi Agosti kufikia asilimia 62 pekee inayotakiwa kwa mgao wa kila siku wa kaloris 2,100. Umoja wa Mataifa pia unaisihi jumuiya ya kimataifa kuchangia fedha ili kuwasaidia zaidi ya wakimbizi milioni mbili wa Sudan Kusini wanaopewa hifadhi katika nchi za jirani huko Afrika mashariki.

XS
SM
MD
LG