Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:42

Wakenya watofautiana juu ya mwezi muwafaka wa kupiga kura


Jengo la Bunge la Kenya
Jengo la Bunge la Kenya

Wananchi wa Kenya wameeleza maoni tofauti juu ya pendekezo la kubadilisha sheria ya siku ya kupiga kura kutoka mwezi Agosti hadi Disemba, wengi wao wakipendelea zoezi hilo lifanyike mwezi Disemba.

Kamati ya Haki na Sheria ya Bunge la Taifa ilikuwa inatembelea miji ya Eldoret na Mombasa kukusanya maoni ya Wakenya juu ya pendekezo la muswada huo.

Timu hiyo pia inatafuta maoni juu ya muswada mwengine wa kuongeza muda wa kufikia sheria ya jinsia ya theluthi mbili baada ya miaka 20. Sheria hiyo inataka kutokuwepo na wajumbe wa jinsia mmoja zaidi ya theluthi mbili katika uteuzi unaofanyika katika taasisi za umma.

“Tunafanya uchaguzi mwezi Agosti na tumeona kile waalimu zetu wanachopitia katika kuhakikisha wanamaliza mtaala kabla ya uchaguzi wa Agosti ili kuepuka kuyumbishwa katika kutoa mafunzo,” amesema Grace Oloo katika Shule ya Serikali, Mombasa.

Katika Katiba ya 2010, Wananchi wa Kenya walikubali kuwa na uchaguzi kila Jumanne ya pili ya mwezi Agosti inapofika miaka mitano.

XS
SM
MD
LG