Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:37

Wahamiaji wa Ulaya watapewa muda wa kuomba hifadhi nchini Ugiriki - EU


Wahamiaji na wakimbizi wakiandamanda kwenye kambi ya muda katika mpaka wa Ugiriki na Macedonia karibu na kijiji cha Idomeni, Ugiriki.
Wahamiaji na wakimbizi wakiandamanda kwenye kambi ya muda katika mpaka wa Ugiriki na Macedonia karibu na kijiji cha Idomeni, Ugiriki.

Umoja wa Ulaya umetoa tangazo la kushangaza kwamba hatimaye kutakuwa hakuna kuwarejesha moja kwa moja wahamiaji kutoka visiwa vya Ugiriki kwenda Uturuki ikiwa ni kuitikia mwito wa watetezi wa haki za binadamu.

Jean-Pierre Schembri ambaye ni msemaji wa idara ya hifadhi ya Umoja wa Ulaya ameiambia VOA kwamba jumuiya hiyo imeamua kuwapa wahamiaji wote haki ya kuomba hifadhi kabla ya kupelekwa nchini Uturuki kwa mujibu wa sera ambayo ilianza kutekelezwa siku ya Jumatatu.

Zaidi ya wahamiaji 200 waliowasili kinyume cha sheria katika kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos walipelekwa Uturuki kwa kubadilishana na raia wa Syria ambao walikuwa wakipatiwa hifadhi katika kambi za Uturuki.

XS
SM
MD
LG