Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 05:14

Wahamiaji 973 waingia Uingereza ndani ya siku moja kupitia baharini


Baadhi ya wahamiaji waliojaribu kuvuka kuingia Uingereza akiwemo mtoto mdogo wakiwa na maafisa wa usalama mjini Dover, kusini mashariki mwa Uingereza Juni 12, 2024.
Baadhi ya wahamiaji waliojaribu kuvuka kuingia Uingereza akiwemo mtoto mdogo wakiwa na maafisa wa usalama mjini Dover, kusini mashariki mwa Uingereza Juni 12, 2024.

Takwimu za Jumapili kutoka wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza zimeonyesha kuwa wahamiaji 973 waliingia nchini humo kupitia mlango wa bahari unaotokea Ufaransa, huku wengine wanne wakifa wakati wa safari hiyo.

Safari hiyo ya Jumamosi imeripotiwa kuvunja rekondi ya wahamiaji wengi zaidi katika siku moja kufanya safari hiyo, wakiwa ni wengi kuliko wale 882, waliovuka na kuingia Uingereza mnamo Juni 18. Siku hiyo mvulana wa miaka 2 na watu 3 wazima walikufa baada ya boti iliyokuwa imejaa kupita kiasi kutatizika wakati wa safari hiyo hatari ambayo maelfu ya wahamiaji hujaribu kuifanya kila wakati.

Mikasa hiyo ya karibuni inafikisha idadi ya watu waliokufa mwaka huu wakijaribu kuingia Uingereza kuwa 51. Zaidi ya wahamiaji 26,600 wameingia Uingereza kwa kupitia mlango huo wa bahari mwaka huu pekee, kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza. Ripoti zimeongeza kusema kuwa vifo vya Jumamosi huenda vilisababishwa na msongamano mkubwa kwenye boti za wahamiaji.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Yvette Cooper amesema kuwa inahuzunisha kuona wahamiaji zaidi wakifa wakati wakijaribu kuingia nchini humo. Kupitia ujumbe wa X, Waziri huyo alisema kuwa magenge ya wahalifu hupanga safari hizo hatari, na wala hawajali iwapo watu watapoteza maisha yao. Serikali mpya ya Labour chini ya waziri mkuu mpya Keir Starmer, inajitahidi sana kudhibiti tatizo la uhamiaji, ambalo lilizungumziwa zaidi kwenye kampeni kuelekea uchaguzi wa Julai.

Forum

XS
SM
MD
LG