Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:20

Wahamiaji 37 waliookolewa kwenye pwani ya Cape Verde warudishwa Senegal


Wahamiaji wawasili Senegal
Wahamiaji wawasili Senegal

Mamlaka nchini Senegal Jumatatu ziliwarudisha nyumbani wahamiaji 37 ambao waliokolewa kwenye pwani ya Cape Verde wiki iliyopita, baada ya boti yao kukwama kwa wiki kadhaa, katika Bahari ya Atlantiki, baada ya  kuishiwa na mafuta.

Walionusurika, haswa kutoka kijiji cha wavuvi cha Fass Boye, walitia nanga Jumatatu jioni. Wengine walitolewa nje ya boti kwa machela, wakiwa dhaifu sana, kuweza kusimama baada ya masaibu yaliyowakumba.

Walikuwa miongoni mwa abiria 101, walioondoka Senegal wakiwa kwenye boti mnamo Julai 10 – ikiwa moja ya boti nyingi ambazo hujaribu kuvuka kutoka pwani ya Afrika Magharibi hadi Visiwa vya Canary, ambavyo hutumiwa na wahamiaji wa Kiafrika wanaojaribu kufika Uhispania.

Mamlaka zilipanga kuwarejesha makwao kutoka kisiwa cha Cape Verde cha Sal, ambapo daktari wa Senegal ambaye alisaidia kutafsiri kati ya walionusurika na mamlaka, alieleza kuwa boti hiyo iliishiwa na mafuta. Ilikuwa imeelea baharini hadi meli ya uvuvi ya Uhispania ilipowapata Agosti 16.

"Wengine walisema ilichukua siku nane, wengine 12. Chakula chao kiliisha haraka sana," daktari, Medoune Ndiaye, aliwaambia waandishi wa habari mjini Sal.

Waziri wa mambo ya nje wa Senegal, Anette Seck, alisema watu 38 waliokolewa kati ya 101, huku miili saba pekee ikiwa imepatikana hadi sasa.

Forum

XS
SM
MD
LG