Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 26, 2024 Local time: 22:57

Wagonjwa tisa wafariki kutokana na moto kwenye hospitali ya Iran


Picha ya maktaba ya wazima moto kwenye hospitali ya Gandhi, Iran Januari 5, 2024
Picha ya maktaba ya wazima moto kwenye hospitali ya Gandhi, Iran Januari 5, 2024

Takriban wagonjwa tisa wamekufa mapema Jumanne, baada moto kuzuka kwenye hospitali iliyopo kwenye mji wa kaskazini mwa Iran, wa Rasht, chombo cha habari cha serikali kimeripoti.

Moto kwenye hospitali ya Ghaem, ulizuka saa saba na nusu za usiku, chombo cha habari cha IRIB kimesema, kikiongeza kuwa ulidhibitiwa, wakati wachunguzi wakifanya kazi ili kufahamu chanzo chake.

“Kwa bahati mbaya tumepoteza watu tisa kwenye mkasa huo,” amesema Mohammad Taghi Ashobi, rais wa Chuo kikuu cha Gilan cha Sayansi ya matibabu. Amesema wagonjwa wengi waliokufa walikuwa wamelazwa katika wadi ya wagonjwa mahututi. Ripoti zinasema kuwa vitanda 142 kati 250 vilivyoko kwenye hospitali hiyo vilikuwa na wagonjwa.

Novemba 2023, moto mkubwa ulizuka kwenye kituo cha kurekebisha watu walioathiriwa na uraibu wa dawa za kulevya kwenye mji wa Langarud, uliopo katika jimbo la Gilan pia, na kuuwa watu 32. Juni 2020, watu 19 walikufa kufuatia mlipuko wa mtungi wa gesi uliosababisha moto kwenye kliniki moja kaskazini mwa Tehran.

Forum

XS
SM
MD
LG