Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 01:35

Wafungwa 260 wanawake walishambuliwa kingono nchini DRC


Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na maeneo yalio jirani nao.
Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na maeneo yalio jirani nao.

Miongoni mwao wasichana  17 walikuwa chini ya umri wa miaka 19. Tukio hili lilitokea Septemba mbili katika jela ya Makala.

Zaidi ya wafungwa wanawake 260 walishambuliwa kingono wakati wa jaribio kutoroka gereza kuu la Makala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwezi huu, ripoti ya ndani ya Umoja wa Mataifa iliyoonekana na shirika la habari la Reuters ilieleza.

Takriban watu 129 waliuawa wakati walinzi wa gereza walipotumia silaha za moto dhidi ya wafungwa wanaojaribu kutoroka gerezani mjini Kinshasa ambapo takwimu rasmi zinasema lina uwezo wa kuhifadhi wafungwa 1,500 lakini lina wafungwa zaidi ya 15,000.

Serikali ilisema baada ya jaribio hilo kutokea nyakati za alfajiri hapo Septemba 2, wanawake walishambuliwa kingono bila ya kutaja idadi kamili. Lakini ripoti ya ndani ya Umoja wa Mataifa iliyoonekana na Reuters kuhusu tukio hilo, ilisema wanawake 268 kati ya 348 waliofungwa katika jela ya Makala wamefanyiwa manyanyaso ya ngono, ikiwemo ubakaji wakati vurugu zilipotokea.

Miongoni mwao wasichana 17 walikuwa chini ya umri wa miaka 19.

Forum

XS
SM
MD
LG