Amesema hayo wakati waokoaji wakijaribu kuwaondoa manusura zaidi kutoka kwenye mabaki hayo.
Waokozi walitumia vifaa maalumu kujaribu kuwafikia watu waliokwama kwenye ghorofa za juu za jengo hilo lenye wakazi 1,700, ambao baadhi yao walitoa ishara ya kuomba msaada kwa taa za simu zao za mkononi.
Shughuli za utafutaji na uokoaji ziliendelea mpaka nyakati za mchana. Rais Zelenskyy aliahidi kupigania kila maisha ya watu waliokumbwa na shambulizi hilo.
Pia alisema watu 73 walijeruhiwa katika shambulio hilo Jumamosi na 39 wameokolewa kufikia Jumapili alasiri.