Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:29

Wafanyakazi wa ubalozi wa Iran watakiwa kuondoka Albania


Kikosi maalumu cha polisi kikiingia Ubalozi wa Jamuhuri ya Kislamu ya Iran, mjini Tirana Septemba 8, 2022. Picha na Florion Goga/REUTERS
Kikosi maalumu cha polisi kikiingia Ubalozi wa Jamuhuri ya Kislamu ya Iran, mjini Tirana Septemba 8, 2022. Picha na Florion Goga/REUTERS

Wafanyakazi wa ubalozi wa Iran, katika mji mkuu wa Albania, walifanya kazi usiku kucha baada ya kupewa saa 24 za kuondoka nchini humo kutokana na shambulizi kubwa la kimtandao ambalo serikali ya Albania, inailaumu Iran.

Hiki ni kisa cha kwanza kinachojulikana kwa nchi hiyo kuvunja uhusiano wa kidiplomasia kutokana na shambulizi hilo.

Harakati ndani ya ubalozi wa Iran mjini Tirana, ziliendelea bila kukoma kuanzia Jumatano hadi Alhamis.

Pipa tupu lilionekana likipelekwa katika eneo hilo na baadae moto ulianza kuwaka ndani yake ikionekana kama ni kuchoma nyaraka.

Gari la kidiplomasia liliingia na kutoka wakati afisa wa polisi wa Albania aliwasiliana na ubalozi huo kabla ya maafisa wawili kuingia na kutoka baada ya dakika chache.

Wafanyakazi walipewa muda wa hadi saa sita mchana leo kwa saa za huko ili kuondoka Albania.

XS
SM
MD
LG