Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 03:08

Wafanyakazi wa kiwanda cha Samsung cha India waitisha mgomo


Baadhi ya wafanyakazi wa Samsung wanaoshiriki kwenye mgomo wa kuitisha nyongeza za mishahara, Chennai, India, Sept. 12, 2024.
Baadhi ya wafanyakazi wa Samsung wanaoshiriki kwenye mgomo wa kuitisha nyongeza za mishahara, Chennai, India, Sept. 12, 2024.

Wafanyakazi 104 kwenye kiwanda cha elektroniki cha Samsung, waliokuwa wakilalamikia mishahara midogo kusini mwa India Jumatatu wamezuiliwa na polisi kwa tuhuma za kupanga maandamano bila kibali, wakati harakati zao zikisemekana kuathiri shughuli kwenye kiwanda hicho kwa wiki moja iliyopita.

Ukamataji huo unabainisha kusambaa kwa mgomo wa wafanyakazi kwenye kiwanda hicho cha kutengeneza vifaa vya nyumbani vya Samsung, kilichoko mjini Chennai kwenye jimbo la Tamil Nadu.

Wafanyakazi hao wanaodai nyongeza ya mishahara huku wakisitisha kazi zao kwenye kiwanda hicho ambacho kinachangia takriban theluthi moja kwa mapato ya mwaka ya India ya dola bilioni 12. Mgomo huo unatia mashaka mpango wa waziri mkuu Narendra Modi wa kuwavutia wawekezaji wa kigeni, ili kutengenezea bidhaa ndani ya India, kwa lengo la kuimarisha uzalishaji wa vifaa vya elektroniki hadi dola bilioni 500 ndani ya kipindi cha miaka sita.

Makampuni mengi ya kigeni huvutiwa na wafanyakazi wanaolipwa mishahara midogo nchini India, na kupata nafasi ya kupanua wigo wao nje ya China. Tangu wiki iliyopita, wafanyakazi wa kiwanda hicho wamekuwa wakikusanyika kwenye hema la muda karibu na kiwanda hicho, wakidai nyongeza ya mishahara, pamoja na kujiunga kwenye muungano wa wafanyakazi wa India wa , CITU.

Forum

XS
SM
MD
LG