Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilitangaza Jumatatu kwamba imekamata ndege na kundi la wafanyabishara magendo wa madini wakijaribu kuondoka kutoka mji wa mashariki wa Goma.
Gavana wa Kivu Kaskazini, Julien Paluku, amesema Wanigeria watatu, Wamarekani wanne na Mfaransa mmoja wamekamatwa. Na wamepatikana na kilo zaidi ya 400 za dhahabu na dola milioni 6 ambazo nyingi zilikua za bandia.
Gavana Paluk anasema watu hao huwenda ni shemu ya mtando wa kimataifa unaofanya biashra ya magendo ya bishara, na wameingia DRc wakati wakijua kwamba Rais Joseph Kabila alipiga marufuku uchimbaji magendo wa madini huko Mashariki ya Kongo tangu mwezi Septemba 2010.