Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:03

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa waiomba mahakama kuhalalisha hati ya kumkamata Rais wa Syria


Rais wa Syria Bashar al-Assad
Rais wa Syria Bashar al-Assad

Waendesha mashtaka wa Ufaransa wameiomba Mahakama ya juu nchini humo kuamua kuhusu uhalali wa hati ya kimataifa ya kumkamata Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Assad anatuhumiwa kuhusika katika uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, ingawa waendesha mashtaka wanakubali kuwa Assad, kama kiongozi wa nchi, anapaswa kuwa na kinga kamili.

Majaji wa mahakama ya rufaa wiki iliyopita waliamua kuwa hati hiyo ya kumkamata Assad ni halali, na kwamba kufikia sasa inatumika. Mawakili wa waathirika wanasema uamuzi wa mahakama ya rufaa ulikuwa “hatua kubwa katika vita dhidi ya kutowaadhibu wahalifu.”

Kulingana na rufaa ya waendesha mashtaka, ni “muhimu kwa mtazamo wa kisheria” kuzingatia kinga kama kiongozi wa nchi kuhusiana na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Waendesha mashtaka wamesema kuwa kinga kwa viongozi wa nchi za kigeni inapaswa kubatilishwa tu na mashtaka ya kimataifa, ikiwemo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Hata kwamba Assad hatahudhuria kesi nchini Ufaransa, hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa dunia ni nadra.

Ufaransa itakuwa ni nchi ya kwanza kutoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa nchi ya kigeni aliye madarakani.

Forum

XS
SM
MD
LG