Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 08:48

Waendesha mashitaka waomba Januari 2, 2024 kuanza kusikilizwa kwa kesi ya jinai dhidi ya Donald Trump


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipofanya mkutano wa kampeni mjini Windham New Hampshire Agosti 8, 2023. REUTERS/Reba Saldanha.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipofanya mkutano wa kampeni mjini Windham New Hampshire Agosti 8, 2023. REUTERS/Reba Saldanha.

Muda kama huo  unaweza kumlazimisha Trump kutumia siku zake za wiki kortini mapema mwaka 2024 wakati ambapo uchaguzi wa kwanza wa uteuzi wa rais wa chama cha Republican umepangwa

Waendesha mashitaka wa wizara ya sheria ya Marekani siku ya Alhamisi waliomba tarehe ya Januari 2 mwaka 2024 ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ya jinai dhidi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anayetuhumiwa kwa kula njama kinyume cha sheria kutaka kubadili matokeo ya kushindwa kwake katika uchaguzi wa mwaka 2020 dhidi ya Joe Biden wa chama cha Democrat.

Katika kesi yake na Jaji wa Wilaya ya Marekani Tanya Chutkan mjini Washington ofisi ya mwendesha mashitaka maalum Jack Smith, ambaye ndio mwendesha mashitaka mkuu katika kesi hiyo ilisema inatarajia uwasilishaji wake wa ushahidi dhidi ya Trump utachukua sio zaidi ya wiki nne hadi sita na uteuzi wa baraza la mahakama kufanyika kabla ya hapo mwezi Desemba.

Muda kama huo unaweza kumlazimisha Trump kutumia siku zake za wiki kortini mapema mwaka 2024 wakati ambapo uchaguzi wa kwanza wa uteuzi wa rais wa chama cha Republican umepangwa kama vile vikao vya chama Januari 15 katika jimbo la Magharibi Kati la Iowa.

Forum

XS
SM
MD
LG