Wakati Sudan inajiandaa kwa kura ya maoni juu ya uhuru wa Sudan kusini , wafuatiliaji wa kimataifa wameanza kuwasili huko kusini mwa Sudan kuangalia jinsi matayarisho yanavyoendelea. Haya yametokea wakati wachambuzi wanahofia kuwa mashauriano ya baina ya upande wa Kaskazini na Kusini yaliyokwama yanaweza kuhatarisha kura hiyo muhimu.
Lakini maafisa wa marekani wanasema pande hizo mbili ziko karibu kuafikiana katika masuala muhimu.
Wafuatiliaji hao kumi na sita wa kimataifa wamepelekwa kutoka kituo cha ufuatiliaji cha Carter chenye makao yake hapa marekani- Carter center, ili kutathmini upigaji kura wa maoni Januari tisa mwakani Kusini mwa Sudan.
Zikiwa zimebaki siku 100 kufanyika uchaguzi huo maandalizi bado yako nyuma ya ratiba. Uandikishaji wa wapiga kura ulitakiwa kumalizika mwezi Agosti na bado haujaanza na wachambuzi wameonya kuwa hiyo inaweza kuchelewesha zoezi hilo la kura na kusababisha ghasia baina ya pande hizo mbili.
Wafuatiliaji wa kimataifa wameanza kuwasili huko kusini mwa Sudan kuangalia jinsi matayarisho yanavyoendelea.