Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 13:19

Wachambuzi Afrika waeleza matumaini kufuatia ushindi wa Biden Marekani


wachambuzi na wanasiasa barani Afrika wamefurahishwa na tangazo la kuwa Joe Biden na Kamala Harris ndio washindi wa uchaguzi mkuu wa urais, Marekani.

wachambuzi na wanasiasa barani Afrika wamefurahishwa na tangazo la kuwa Joe Biden na Kamala Harris ndio washindi wa uchaguzi mkuu wa urais, Marekani.

Wachambuzi hao na wasiasa sasa wametoa orodha ndefu ya mambo ambayo utawala ujao unastahili kuweka kipaumbele kwa bara la Afrika.

Taarifa kutoka kwa wakfu wa Nelson Mandela inasema kwamba imefurahishwa sana na kushindwa kwa rais Donald Trump na kwamba wana furaha kuwa hawataendelea kuona taasisi za demokraisia zikikandamizwa kwa miaka mingine minne.

Mandela alikuwa rais wa kwanza mwafrika, kuongoza Afrika kusini. Utawala wake umepata sifa nyingi kiasi cha kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kumuweka upande tofauti na baadhi ya marais wa hivi karibuni nchini Marekani.

Mkurugenzi wa wakfu wa Mandela Sello Hatang amesema, “Mambo ambayo rais Trump amefanya bahati mbaya yalikuwa ambayo tusingependa kuona tena katika nchi hiyo kubwa. Kuongezeka kwa chuki lilikuwa linaanza kuwa jambo la kawaida na kuweka mazingira ya kushambulia wenzako kwa maneno hata wapinzani wa kisiasa bila kujali ni akina nani, hakukuwa na uongozi.

Watu wengi nchini Afrika kusini wamefurahishwa na ushindi wa Joe Biden. Rais Cyril Ramaphosa, amempongeza Biden na Haris kwa ushindi huo.

Hata hivyo chama chenye mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters - EFF, kimesema kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu Marekani, huenda yasiwe na mabadiliko makubwa kwa wamarekani wenye asili ya Afrika na kwamba wataendelea kubaguliwa.

Sarfo Abebrese, mtetezi wa maslahi ya Afrika, ambaye pia ni wakili, raia wa Ghana, anasema kwamba ana furaha ya kutoa orodha ya mambo ambayo utawala mpya wa Marekani unastahili kushughulikia kwa ajili ya Afrika.

“Tunatarajia kwamba utawala wa Joe Biden utawasikiliza waafrika. Tunataka demokrasia katika nchi nyingi za Afrika. Tuna viongozi wengi wa Afrika wanavunja sheria na kujichukulia madraka, waking’ang’ania madarakani kwa miaka 10,20,30. Tunataka mfumo wa kidemokrasia kama wa Marekani kujengwa Afrika. Unaanzia juu.” Amesema Sarfo Abebrese

Bara la Afrika halikutajwa sana wakati wa Kampeni za Marekani. Biden ana wanawake wawili katika ngazi ya juu ya uongozi wake kama washauri wake.

Hatang anasema hii ni ishara njema.

“Tuna matarajio kwamba hali hii inaweka mwelekeo kwa Afrika kusini kwamba hatutakuwa na aibu kumteua rais mwanamke. Tukiwa na uongozi kama huu, tutapata fursa ya jambo hilo kutokea hapa Afrika kusini.”

Professor Ina Gouws wa chuo kikuu cha Free State, Afrika kusini amefurahishwa na ushindi wa kihistoria wa Harris na kusema kwamba Marekani inaonekana inataka kuzingatia sana bara la Afrika na wanastahili kuonyesha kwamba wanajali kwa kuleta maendeleo kupitia uwekezaji.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG