Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:37

Wachache wajitokeza kupiga kura Tunisia


Muungano wa upinzani nchini Tunisia umetoa mwito wa kuungana dhidi ya rais Kais Saied, baada ya raia wa Tunisia waliojitokeza katika duru ya pili ya kura Jumapili kwa bunge lisilokuwa na nguvu kuwa ni asilimia 11.3 katika taifa lililogawanyika.

Ahmed Naejib Chebbi, mkuu wa chama cha National Salvation Front, aliwaeleza wanahabari kwamba takriban asilimia 90 ya wapiga kura wa Tunisia walipuuzia kura na kukataa kujihusisha katika mchakato.

Amesema anatoa mwito kwa makundi yote ya kisiasa na kiraia kuungana kuleta mabadiliko ya kumuondoa rais Kais Saied, na uchaguzi wa mapema wa urais.

Kufuatia hali kama hiyo ya waliojitokeza katika duru ya kwanza, kujitokeza kwa kiwango kidogo kwa watu Jumapili imekuwa ni mbaya kwa rais Saied, ambaye ameliweka bunge chini ya mamlaka yake na kujipatia nguvu toka kutwaa madaraka mwaka 2021 katika kitovu cha vuguvugu la Kiarabu.

XS
SM
MD
LG