Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 04:06

Wamarekani weusi wapinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu


Sen. Cory Booker, Mdemokrat -N.J na Mwakilishi John Lewis, Mdemokrat - Georgia wakitoa ushuhuda Capitol Hill, Jan. 11, 2017.
Sen. Cory Booker, Mdemokrat -N.J na Mwakilishi John Lewis, Mdemokrat - Georgia wakitoa ushuhuda Capitol Hill, Jan. 11, 2017.

Seneta Sessions atatakiwa kutekeleza sheria ya haki sawa kwa wanawake, kulinda haki za upigaji kura na haki sawa kwa wote lakini rekodi yake inaonyesha hana msimamo huo

Wabunge weusi wa chama cha Demokratik wenye ushawishi, Jumatano walitoa ushahidi wao unaopinga uteuzi wa Seneta wa Republika, Jeff Sessions aliyeteuliwa na rais mteule kuwa mwanasheria mkuu ajaye wa Marekani.

Kama atathibitishwa, seneta Sessions atatakiwa kutekeleza sheria ya haki sawa kwa wanawake, lakini rekodi yake inaonyesha hana msimamo huo, alisema seneta wa mdemokratik, Cory Booker wa New Jersey, mbele ya kamati ya sheria katika baraza la seneti, ambayo inasikiliza uteuzi wa Sessions.

Kadhalika ameeleza kuwa atatarajiwa kulinda haki sawa za wamarekani mashoga na wale waliobadili jinsia zao, lakini rekodi yake inaonyesha hakubaliani na hilo.

Kwa upande wa upigaji kura mteule huyu atatarajiwa kulinda haki za upigaji kura, lakini amesema rekodi yake pia inaonyesha msimamo wake ni kinyume cha hilo.

Muda mfupi baadaye mbunge wa Demokratik, John Lewis, kiongozi wa kundi la haki za kiraia, alisema Marekani imepiga hatua kubwa kuelekea usawa na sheria, lakini bado hatujafikia huko. Alisema hivyo tunataka kusonga mbele.

XS
SM
MD
LG