Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 16:42

Waasi 'waua' takriban raia 20 DRC


DRC and Uganda
DRC and Uganda

Wanamgambo wa Kiislamu  wanatuhumiwa kuua takriban raia 20  kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo majira ya usiku.

Wanamgambo wa Kiislamu wanatuhumiwa kuua takriban raia 20 kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo majira ya usiku.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa raia wa ndani na mwanaharakati ambaye amekosoa kushindwa kwa vikosi vya Congo na Uganda kuzuia mauaji hayo.

Shambulizi la Jumapili jioni katika kijiji cha Kikura lililaumiwa na mkazi na mwanaharakati wa ADF, mwanamgambo wa Uganda ambaye ameuwa maelfu ya raia mashariki mwa Congo tangu mwaka 2013.

Vikosi vya Congo na Uganda vilianzisha operesheni za pamoja dhidi ya ADF mwishoni mwa Novemba lakini mashambulizi ya kundi hilo ambalo limedai kuwa na uhusiano na Islamic state limeendelea kuuwa dazani za raia kila mwezi.

Washambuliaji hao walivamia kwa kutumia mapanga , kuchoma moto nyumba, alisema Odette Zawadi rais wa shirika la wanaharakati wa ndani. Amesema miili 20 imepatikana na kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

XS
SM
MD
LG