Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:25

Waasi wa M23 wamesema wapo tayari kwa mapigano baada ya serikali ya DRC kusema hakuna nafasi ya mazungumzo


Waasi wa M23 wakitembea katika mji wa Karuba, kilomita 62 kutoka Goma, kivu kaskazini, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Waasi wa M23 wakitembea katika mji wa Karuba, kilomita 62 kutoka Goma, kivu kaskazini, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema haitafanya mazungumzo na kundi la waasi la M23, baada ya kundi hilo kusema kwamba lipo tayari kwa mazungumzo hayo.

Msemaji wa DRC Patrick Muyaya amesema ni wazi kwamba serikali haitafanya mazungumzo na kundi la M23. Muyaya amesema kundi la M23 ni kundi la kigaidi na kwamba serikali ya Kinshasa haiwezi kushirikiana na kundi kama hilo.

Msimamo wa DRC unajiri wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki inajitayarisha kutuma jeshi la pamoja katika sehemu za Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika vita dhidi ya makundi ya waasi yaliyo sehemu hiyo likiwemo kundi la M23.

Msemaji wa kundi hilo Meja Willy Ngoma amesema kwamba hawataweka chini silaha.

“Ile ni ndoto. Hatuwezi kamwe kuweka silaha chini. Haiwezekani. Ile ni ndoto kabisa. Hatuwezi kuwaacha kupigana kwa sababu sisi tunapenda mazungumzo. Lakini kama serikali ya Congo haitaki mazungumzo, na sisi tupo tayari kwa mapambano sasa. Tutapigana kabisa kwa kujilinda na tutapigana vizuri sana. Tutawafuata kila sehemu watakwenda wasituharibie amani yetu. Tutawanyang’anya hizo silaha zao,” amesema msemaji wa waasi wa M23 meja Willy Ngoma.

M23 wamesema hawataondoka Bunagana

Mapema mwaka huu, kundi la M23 lilidhibiti mji wa Bunagana ulioko kwenye mpaka na Uganda na limesema kwamba linalinda jamii ya Watutsi dhidi ya mashambulizi ya kundi la wapiganaji la FDLR ambalo ni la wahutu, limetuhumiwa kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kimepangiwa kuongozwa na wanajeshi wa Kenya.

Meja Ngoma ameiambia Sauti ya Amerika kwamba kundi la M23 siyo adui wa jeshi la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki na jeshi hilo likiingia DRC, litakuwa linatafuta adui wao na wala siyo kundi la M23, namna jeshi la Uganda linapambana na kundi la Allied Democratic Forces ADF na Burundi wanavyopambana na kundi la Red Tabara.

Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (FARDC) nlikipiga doria Rutshuru, Kiuvu kaskazini. Novemba 4 2013 4
Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (FARDC) nlikipiga doria Rutshuru, Kiuvu kaskazini. Novemba 4 2013 4

“Jeshi la Kenya litakuja kutafuta amani pekee yake. Kitakuwa kikosi cha kuingilia kati kusuluhisha mzozo. Kikosi hicho hakiji kupigana na M23. Wanajua sababu inayofanya tunapigana,” amesema Willy Ngoma, akiongezea kwamba “Sisi hatutatoka Bunagana. Tupo Bunagana, tutabaki pale. Hakuna nguvu yoyote inaweza kututisha na hakuna kitu chochote kinatutisha. Jeshi lolote litakalokuja kututisha, tutakabiliana nalo. Tuna uwezo na tuna hiyo nguvu. Bunagana hatuwezi kuondoka na hakuna nguvu itatutoa. Sisi tupo tayari kwa mazungumzo lakini kwa nguvu, haitawezekana.”

Kundi la M23 vile vile lianataka rais wa DRC Felix Tshisekedi kuliruhusu kufanya kazi kama kikosi maalum cha jeshi Mashariki mwa DRC.

Rais Tshisekedi amefanya mabadiliko katika jeshi la DRC na kuwaondoa makamanda ambao walihusishwa na ukosefu wa usalama pamoja na ufisadi Mashariki mwa DRC.

Serikali ya Rwanda imeshutumiwa kuliunga mkono kundi la M23, madai ambayo rais Paul Kagame na serikali yake wamekanusha.

Tshisekedi na Kagame walikutana New York

Rais wa Rwnda Paul Kagame (kushoto), Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (katikati) na Félix Tshisekedi (kulia) walipokutana katika umoja wa mataifa, New York, 21 Sept 2022
Rais wa Rwnda Paul Kagame (kushoto), Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (katikati) na Félix Tshisekedi (kulia) walipokutana katika umoja wa mataifa, New York, 21 Sept 2022

Katika mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Septemba mjini New York, Marekani, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, alisema Rwanda ndio inafadhili waasi wa M23 Mashariki mwa Congo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame, akimjibu Tshisekedi, alisema kwamba tatizo la DRC ni la kisiasa na linahitaji suluhu ya kisiasa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikutana na marais hao wawili na kukubaliana kumaliza uhasama.

XS
SM
MD
LG