Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:00

Waasi 33, wanajeshi 2 wauawa katika mapigano makali DRC


Eneo la Ituri, lenye utajiri mkubwa wa mali asili, limeshuhudia mapigano  mabaya zaidi yakitokea kati ya mwaka 1999 na 2007, baada ya mzozo wa madaraka kati ya makundi ya waasi na kupelekea mapigano ya kikabila kati ya makabila ya Hema na Lendu.

Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo limesema kwamba limewaua wapiganaji 33 na kupoteza wanajeshi wawili katika mapigano makali kukomboa sehemu zilizokuwa zimeshikiliwa na makundi ya wapiganaji.

Mapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku nne katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa DRC.

Walinda usalama wa Umoja wa Mataifa wamelisaidia jeshi la Congo kuzuia mashambulizi ya kundi la waasi la CODECO, waliojaribu kuingia mjini Bunia, siku ya Jumamosi.

Kundi la CODECO, ambalo wapiganaji wake wengi wanatoka kabila la Lendu, linashutumiwa na Umoja wa Mataifa kwa mauaji, kukata watu vichwa, kunajisi wanawake na uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Mapigano yamepungua katika baadhi ya sehemu za mashariki mwa DRC baada ya baadhi ya makundi ya wapiganaji kutangaza kusitisha vita mnamo mwezi Agosti, baada ya waliokuwa viongozi wa makundi ya wapiganaji katika eneo hilo kuwaomba kusitisha vita.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema kwamba waasi wa CODECO, watiifu kwa kiongozi wao wanaojulikana kama “Mountain Wolf” walishambulia kituo cha kijeshi karibu na mji wa Dele, kilomita 6 kutoka mjini Bunia.

“Walitaka kuwapa funzo wanajeshi wetu lakini waliumia sana,” amesema msemaji wa jeshi la DRC Jules Ngongo.

Eneo la Ituri, lenye utajiri mkubwa wa mali asili, limeshuhudia mapigano mabaya zaidi yakitokea kati ya mwaka 1999 na 2007, baada ya mzozo wa madaraka kati ya makundi ya waasi na kupelekea mapigano ya kikabila kati ya makabila ya Hema na Lendu.

Baada ya mwongo mmoja wa utulivu, mapigano ya kulipiza kisasi yalianza tena Desemba 2017 na kufufua migogoro iliyokuwepo kuhusiana na umiliki wa ardhi.

Hali hiyo imesababisha wapiganaji wa kundi la CODECO kuimarisha mashambulizi dhidi ya jeshi na kabila la Hema.

Tangu Juni 2018, maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao katika mkoa wa Ituri kutokana na mashambulizi ya makundi ya waasi.

Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kutoroka makwao kutokana na mashambulizi hayo.

Imetayarishwa na Kennes bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG