Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 21:04

Waandishi wa Reuters washikiliwa Myanmar


Jeffrey Feltman (Kati), Makamu wa Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya siasa, akihutubia Baraza la Usalama juu ya hali ya Myanmar.
Jeffrey Feltman (Kati), Makamu wa Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya siasa, akihutubia Baraza la Usalama juu ya hali ya Myanmar.

Waandishi wawili wa Shirika la Habari la Reuters wamekamatwa nchini Myanmar kwa kushukiwa kuwa “wananyaraka za siri za polisi” zinazohusiana na mgogoro wa wakimbizi katika jimbo la Rakhine, serikali imesema Jumatano.

Mwandishi wa habari Wa Lone na Kyaw Soe Oo walikamatwa baadae Jumanne katika mji mkuu wa Yangon na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kuvunja Sheria Rasmi ya Siri.

Waandishi hao wanadaiwa kuwa walipanga “kutuma nyaraka hizo za siri muhimu zinazohusiana na vikosi vya usalama katika jimbo la Rakhine kwa mashirika ya kigeni nje ya nchi” kwa mujibu wa Baraza la Habari la serikali ya Myanmar.

Msemaji wa serikali Zaw Htay amesema maafisa wa polisi” wanaohusika na kesi hiyo” pia walikamatwa na serikali” itawachukulia hatua dhidi yao na waandishi.

Msemaji wa Reuters amesema Abbe Serphos amesema taasisi za habari kwa “haraka zinaomba kupewa taarifa zaidi juu ya mazingira ya kukamatwa kwao na hali yao ilivyo hivi sasa.”

Ubalozi wa Marekani huko Myanmar, ambayo pia nchi hiyo inajulikana kama Burma, imesema, “Tunawasiwasi na kuendelea kuwepo ukamataji usio wakawaida wa Waandishi wa Reuters baada ya kwamba walikaribishwa kukutana na maafisa wa polisi huko Yangon usiku wa jana. Ili demokrasia ipige hatua na kufanikiwa, wanahabari wanatakiwa wawe na uhuru wa kufanya kazi zao.

Tunapendelea kuwa serikali itoe maelezo juu ya ukamataji wa waandishi hawa na kuruhusu mawasiliano nao mara moja.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeeleza katika ujumbe wake wa tweet kuwa “ Uhuru wa habari ni msingi wa demokrasia.

XS
SM
MD
LG