Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:32

Waandishi wa habari wawili washinda tuzo ya amani ya nobeli


Mhariri wa Novaya Gazeta Dmitry Muratov, kushoto, na Mkurugenzi Mtendaji wa Rappler na Mhariri Mtendaji Maria Ressa. Siku ya Ijumaa, Oktoba 8, 2021 wamepata tuzo ya amani ya Nobeli.
Mhariri wa Novaya Gazeta Dmitry Muratov, kushoto, na Mkurugenzi Mtendaji wa Rappler na Mhariri Mtendaji Maria Ressa. Siku ya Ijumaa, Oktoba 8, 2021 wamepata tuzo ya amani ya Nobeli.

Waandishi wa habari wawili ambao kazi yao imewakasirisha maafisa wa serikali za Russia  na Ufilipino ni washindi wa Tuzo ya amani ya Nobeli  ya mwaka huu wa 2021

Waandishi wa habari wawili ambao kazi yao imewakasirisha maafisa wa serikali za Rashia na Ufilipino ni washindi wa tuzo ya amani ya Nobeli ya mwaka huu 2021, ikiwa ni heshma kuu kwa haki ya uhuru wa kujieleza ambayo kamati ya kutoa tuzo ilitaja kuwa iko hatarini kote ulimwenguni.

Maria Ressa wa Ufilipino na Dmitry Muratov wa Russia walipewa tuzo hiyo kwa vita vyao kwa ujasiri kutetea uhuru wa kujieleza katika nchi zao. Mwenyekiti wa Kamati ya Nobel ya Norway Berit Reiss-Andersen aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Aliongeza kusema kwamba “wakati huo huo, wao ni wawakilishi wa waandishi wote wanaotetea msimamo huu katika ulimwengu ambao demokrasia na uhuru wa wanahabari wanakabiliwa na hali mbaya.”

Tuzo hiyo ni ya kwanza kwa waandishi wa habari tangu Mjerumani Carl von Ossietzky aliposhinda mwaka 1935 kwa kufichua mpango wa siri wa kutengeneza silaha baada ya kumalizika vita wa nchi yake.

Uandishi wa habari huru, na unaofuata msingi ya ukweli hutumika kulinda dhidi ya matumizi mabaya ya nguvu, uwongo na propaganda za vita, Reiss-Andersen alisema.Muratov ni mhariri mkuu wa gazeti la uchunguzi la Russia Novaya Gazeta, ambalo limepinga Kremlin chini ya Rais Vladimir Putin na uchunguzi wa makosa na ufisadi, na kuandika kwa kiasi kikubwa kuhusu mzozo huko Ukraine.

Ni Mrussia wa kwanza kushinda tuzo ya amani ya Nobeli tangu kiongozi wa Soviet Mikhail Gorbachev ambaye yeye mwenyewe alisaidia kuanzisha Novaya Gazeta na pesa alizopokea kutoka kushinda tuzo hiyo mwaka 1990.

Ressa anaongoza Rappler, kampuni ya habari ya mtandao ambayo aliianzisha mnamo 2012, na ambayo imekua maarufu kupitia ripoti za kiuchunguzi, ikiwa ni pamoja na ripoti za mauaji makubwa wakati wa kampeni ya polisi dhidi ya dawa za kulevya.

XS
SM
MD
LG