Baghdad imerudi katika hali yake ya kawaida baada ya kutoka kwenye ukingo wa mzozo wa kisiasa. Waandamanaji wanaopinga Serikali ambao walivamia jengo la Bunge la Iraq waliondoka kwa amani baada ya matangazo kutolewa kuwataka waondoke.
Jumamosi waandamanaji walioongozwa na kiongozi wa kishia Moqtada al Sadr walimiminika mitaani mbele ya bunge la nchi hiyo na kuingia kwa wingi katika eneo lijulikanalo kama Green Zone au International Zone ambako ndiko yaliko majengo ya serikali na balozi kadhaa.
Waandamanaji walifanya uharibifu mkubwa ndani ya jengo la bunge wakati wa maandamano yao ya siku nzima, wakiwa wamejaza mifuko yao na kubeba bendera ambazo baada ya kuondoka kwa amani Jumapili. Baada ya waandamanaji kuondoka, familia zilionekana zikitembea katika eneo hilo, wakipiga picha katika bustani nzuri za eneo hilo.