Polisi walijaribu kuwatawanya karibu waandamanaji 500 waliokuwa wakiwasilisha malalamiko yao ya kupinga mswaada huo bungeni.Mswaada huo unalenga kuongeza kodi ya mafuta na makazi.
Rais William Ruto alishinda uchaguzi wa Agosti mwaka jana kutokana na ahadi za kusaidia watu wa kipato cha chini, lakini sasa hivi anaonekena kukabiliwa na shinikizo la kuongeza mapato ya serikali ili kukabiliana na deni kubwa lililopo.
Hata hivyo pendekezo lake la kuongeza ushuru linakosolewa vikali na wafanyakazi wa serikali pamoja na viongozi wa upinzani ambao wanasema kwamba gharama ya maisha tayari ipo juu zaidi
Forum