Hali hiyo pia ilishuhudiwa kwenye miji mingine ikiwa ni maandamano mengine ya kuupinga utawala wa jeshi kwa mujibu wa chama cha madaktari na mashuhuda.
Takriban watu 60 wamefariki, huku wengine zaidi wakijeruhiwa katika msako wa waandamanaji toka kufanyika kwa mapinduzi mwezi Oktoba ambayo yameharibu juhudi za kuleta mabadiliko ya kidemokrasia kwa mujibu wa chama cha madaktari ambacho kinashirikiana na waandamanaji katika vuguvugu hilo.
Watu walio uwawa Alhamisi wote walikuwa waandamanaji na walifariki kutokana na risasi zilizo fyatuliwa na wana usalama wakati wa maandamano katika miji ya Omdurman na Bahri kuvuka mto Nile kutoka Khartoum kamati kuu ya madaktari wa Sudan imesema