Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:54

Waandamanaji Manila wapinga ziara ya Trump


Waandamanaji mjini Manila wakiwa wanaelekea Ubalozi wa Marekani kupinga ziara ya Rais Trump nchini Ufilipino alipowasili kuhudhuria mikutano ya viongozi wa Bara la Asia na Marekani.
Waandamanaji mjini Manila wakiwa wanaelekea Ubalozi wa Marekani kupinga ziara ya Rais Trump nchini Ufilipino alipowasili kuhudhuria mikutano ya viongozi wa Bara la Asia na Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump amewasili Jijini Manila Jumapili kuhudhuria mikutano ya viongozi wa Bara la Asia na Marekani akiwa na shauku kubwa.

Ndege ya Trump ya Air Force One iliwasili Manila muda mfupi kabla ya saa kumi na mbili jioni, majira ya nchi hiyo, baada ya takriban waandamanaji wa Ufilipino 3,500 kufanya jaribio la kuandamana kwenda Ubalozi wa Marekani.

Waandamanaji hao walipiga kelele wakimtaka Trump kuondoka nchini humo na kuishutumu serikali ya Marekani, mkoloni aliyeikandamiza Ufilipino kwa kiasi cha miaka 50, ikianzisha vita nje ya nchi yake.

“Tunajua kuwa Marekani imekuwa ikianzisha vita duniani kote, na wanajaribu kuvamia nchi zote za ulimwengu wa tatu,” amesema mwanadamanaji Kristine Cabardo, 23. Amedai kuwa ubeberu wa Marekani kitu cha kwanza unaleta vita tu na maangamizi.

Maelfu ya askari wa kuzuia fujo nchini Ufilipino waliwazuia waandamanaji hao, ambao walikuwa wamehamasishwa na chama cha kisiasa cha mrengo wa kushoto.

Waandamanaji hao walidhamiria kufika katika ubalozi wa Marekani au eneo lolote ambalo Trump alikuwa amepangiwa kwenda kuhudhuria mikutano iliyokuwa imeandaliwa na Jumuiya ya Nchi za Kusini-Mashariki mwa Bara la Asia unaoendelea hadi Jumanne.

“Ukweli ni kuwa serikali ya Ufilipino haishughulikii maslahi ya watu wake,” Cabardo amesema.

“Hata wanajeshi na jeshi la polisi hawako kwa ajili ya kulinda na kuwahudumia wananchi. Wao wanatumikia na kuwalinda wale walioko kwenye madaraka, Utawala wa Marekani na Duterte, utawala wa kibaraka wa serikali hii,” alisema mwandamanaji huyo.

XS
SM
MD
LG