Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:22

Vyama vya upinzani vyaongoza kwenye uchaguzi wa Somaliland


Watu wabeba mabango wakati wa kampeni kwelekea uchaguzi wa Somaliland
Watu wabeba mabango wakati wa kampeni kwelekea uchaguzi wa Somaliland

Tume ya taifa ya uchaguzi katika Jamhuri iliyojitenga ya Somaliland imesema Jumapili kuwa vyama viwili vya upinzani vimeshinda viti vingi vya bunge katika uchaguzi wa kwanza kufanyika baada ya miaka 16.

Kati ya viti 82, chama cha Somaliland National Party - WADDANI, kimepata viti 31 huku kile cha Justice and Welfare, UCID, kikipata viti 21. Chama tawala cha Unity and Development, Kilumiye nacho kimejipatia viti 30, tume ya uchaguzi imesema.

Uchaguzi wa ubunge ulicheleweshwa kwa zaidi ya muongo mmoja kutokana na mzozo kati ya vyama vikuu vitatu vya siasa kuhusu muundo kwa tume ya uchaguzi, lakini suala hilo hatimaye limetatuliwa.

Kupitia taarifa ya pamoja, vyama vya WADDANI na UCID vimetangaza muungano wa kisiasa utakaochagua spika wa bunge la Somaliland. Vyama hivyo viliwili pia vinasemekana kuongoza kwenye idadi ya viti vya manispaa vikisema kuwa vitashirikiana katika kuchagua mameya wa miji, pamoja na viongozi wa mabaraza.

Mtayarishi - Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG