Rais wa Russia Vladimir Putin anatarajiwa kushinda muhula mwingine wa miaka sita leo Jumapili katika uchaguzi ambao hakuna upinzani wa kweli, hata wakati baadhi ya Wa-Russia walijitokeza katika vituo vya kupigia kura kote nchini humo kufanya maandamano dhidi ya ushindi wake wa uhakika.
Putin mwenye umri wa miaka 71 anatarajiwa kuongeza utawala wake wa karibu robo karne kwa miaka mingine sita baada ya ukandamizaji mkali dhidi ya wapinzani ambao umeshuhudia waandishi wa habari wakifungwa jela, na kifo kilichotokea Februari cha kiongozi maarufu wa upinzani nchini Russia, Alexey Navalny.
Uchaguzi huo, ambao ulianza Ijumaa, umefanyika bila ya upinzani wowote wa kweli au mbadala wa Putin. Hata hivyo, watu kadhaa walijitokeza katika vituo vya kupigia kura kote nchini Russia leo Jumapili kushiriki katika kile ambacho upinzani dhidi ya Kremlin, ulisema ni maandamano ya mfano ya kuchaguliwa tena kwa Putin.
Forum