Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:00

Viwavi jeshi wavamia Uganda


viwavi jeshi wakiwa kwenye mimea
viwavi jeshi wakiwa kwenye mimea

Serikali ya Uganda imesema kwamba imetuma maafisa wanaotumia dawa maalum za kuua wadudu, kukabiliana na viwavi jeshi ambao wamevamia wilaya 35 nchini humo.

Uganda ni mzalishaji mkubwa wa mahindi, na huuza nafaka hiyo kwa nchi jirani za Sudan kusini, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Kenya.

Viwavi jeshi wamevamia mashamba kadhaa ya mahindi n akusababisha uharibifu mkubwa, baada ya mvua kuchelewa na kupelekea shughuli ya upanzi kuchelewa.

Wizara ya kilimo ya Uganda imesema kwamba uharibifu wa wadudu hao ni wa kiwango kikubwa na kwamba viwavi jeshi wameendelea kuhama hama kwa kasi kutoka wilaya moja haadi nyingine.

Wilaya zizilo mashariki mwa Uganda, katikati na kaskazini ndizo zimeathiriwa vibaya na wadudu hao.

Kando na mahindi, viwavi jeshi wameharibu mtama, mawele na nyasi kwa ajili ya mifugo.

Taarifa ya wizara ya kilimo haijasema kiasi cha lita za dawa kwa ajili ya kuua wadudu hao, zkimenunuliwa.

XS
SM
MD
LG