Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 09:30

Mahakama kuu DRC yaanza kusikiliza kesi ya Khamere.


Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila alipokuwa akipiga kura.
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila alipokuwa akipiga kura.

Vitali Khamere apeleka mashtaka mahakama kuu akiomba matokeo ya uchaguzi yafutwe.

Mahakama kuu ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeanza kusikiliza kesi ambayo inaomba kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi ambayo yamemrudisha Rais Joseph Kabila madarakani.

Mgombea wa upinzani Vitali Khamere ambaye alimaliza wa tatu katika uchaguzi huo alifikisha mashtaka mahakamani akidai kwamba kura ziliibiwa ili kumpendelea Kabila.

Bw. Kamerhe ambaye alikuwako mahakamani jana wakati wa kesi hiyo alisema baadhi ya karatasi za kura zilikuwa zimetiwa alama kabla kwa ajili ya rais, na kusema tume ya uchaguzi iliripoti matokeo ya uwongo.

Bw. Tshisekedi amekataa matokeo ya uchaguzi huo na kujitangaza rais.

XS
SM
MD
LG